Afisa masoko wa kampuni hiyo Moses Vikael akizungumza katika mbio za Redcross Marathon Arusha zilizofanyika katika uwanja wa Stadium jijini Arusha .

Happy Lazaro,Arusha.

Arusha.Wananchi wametakiwa kutumia bidhaa za umeme jua kutoka kampuni ya teknolojia ya ZOLA ELETRIC kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwani bidhaa hizo zina ubora wa hali ya juu .

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Afisa masoko wa kampuni hiyo Moses Vikael wakati akizungumza katika mbio za Redcross Marathon Arusha zilizofanyika katika uwanja wa Stadium jijini Arusha .

 “Tunafanya kazi ya uuzaji na usambazaji wa sola katika maeneo mbalimbali nchini kupitia mtandao wa mawakala wetu, kuanzia mijini hadi vijijini, na katika sekta zote za biashara, taasisi na makazi ya wananchi.”amesema Moses.

“Lengo letu ni kuhakikisha kila eneo lenye uhitaji wa nishati linapata suluhisho bora la umeme wa jua kutoka kampuni yetu “amesema Moses.

Moses ameongeza kuwa,kitendo hicho kilichofanywa na Redcross ni mfano wa kuigwa kwani kwa mara ya kwanza wameweza kufanya mbio hizo kwa mkoa wa Arusha jambo ambalo limeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Arusha .

“Tunashukuru sana kwa namna ambavyo.Redcross mmeweza kutupa mwaliko wa kuwa wafadhili katika jambo hili na tunawaahidi kuendelea kushirikiana na nyie katika kila hatua “amesema Moses.

Aidha ametoa wito kwa wananchi mbalimbali kiwa na tamaduni za kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao kwani michezo ni afya na inasaidia kuondokana na maradhi mbalimbali ambayo yangeweza ku

tokea .