" WATANZANIA WAHIMIZWA KUENDELEA KULINDA AMANI

WATANZANIA WAHIMIZWA KUENDELEA KULINDA AMANI

 

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa Watanzania waendelee kulinda amani ili nchi iendelee kutekeleza mipango ya maendeleo. 

Dk. Nchemba alisema hayo aliposhiriki ibada kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dayosisi ya Mashariki na Pwani mkoani Dar es Salaam jana.

 Dk. Mwigulu alisema amani ya wananchi inategemea amani manufaa ya wananchi. ya eneo walilopo na akahimiza kuendelea kuliombea taifa. Alisema dunia inapitia changamoto na misukosuko ya kiusalama, hivyo amani ya nchi ni msingi muhimu wa maendeleo na utekelezaji wa mipango ya serikali. 

“Amani ndiyo msingi wa maendeleo. Miradi yote ya serikali na mipango ya maendeleo inaweza kutekelezwa vizuri ikiwa nchi yetu itaendelea kuwa na amani, hivyo ni muhimu kuendelea kuiombea nchi yetu,” alisema. 

Aliongeza: “Leo hii tuna mipango mbalimbali kama nchi, ndani ya familia, usharika, dayosisi, kanisa lakini hayo yote tunaweza kuyafanya kama nchi yetu ina amani”. Dk Mwigulu alisema kanisa lina mchango mkubwa katika maendeleo nchini na serikali inatambua mchango wa kanisa katika kujenga maadili, mshikamano ndani ya jamii na ujenzi wa miradi ya kijamii. 

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini ili kuwezesha nchi kusonga mbele kimaendeleo kwa Dk Mwigulu alichangia Sh milioni 10 kusaidia watu wenye mahitaji na Sh milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa KKKT Mikocheni A. 

Katika ibada hiyo, Dk Mwigulu alifuatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Aggrey Mwanri, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Mbunge wa Makete, Festo Sanga.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post