" WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA WATUMISHI HOUSING

WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA WATUMISHI HOUSING



Watanzania wametakiwa kuwekeza kwenye mfuko wa Faida Fund kwa njia ya e-wekeza ili kuwawezesha kuwa na utamaduni wa kuwa na mitaji kwenye masoko ya mitaji na fedha.

Akizungumza leo kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza, Ofisa Mauzo wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments Kennedy Mkula aliwahimiza watu kuwekeza kwa ajili yao na watoto.

Alisema kupitia mfuko huo mwananchi anakuwa na fursa ya kuweka akiba polepole na hivyo kuweza kukuza mtaji wake ambapo katika muda wa mwaka unapata riba ya asilimia 13.

Mkula alisema mfuko huo unaweza kunufaisha watu wote kuanzia wale wenye vipato vya chini hiku ikimwezesha mnufaika kutumia vipande vyake kama rehani kwa ajili ya kupata mikopo.

"Gharama ya kuwekeza ni inaanzia shilingi 10,000/= na kwa uwekezaji unaofatia ni kuanzia 5,000/= na kuendelea" alisema Mkula.


Wakati huo Watumishi Housing Investments wanatoa huduma za kuuza nyumba zake kwa watanzania wote ambapo kwa watumishi wastaafu wanaweza kutumia malipo yao ya pensheni asilimia 50 kwa kutanguliza na hivyo kuweza kumiliishwa nyumba. 

Alisema kupitia huduma hizo zinazotolewa kupitia uuzaji wa nyumba zilizokamilika humwezesha mtumishi kuweza kumiliki nyumba yake na hivyo kuondokana na upangaji.

Taratibu zote za uwekezaji zimerahisishwa ambapo hufanyika kwa njia ya mtandao mtu akiwa mahali popote.

Mkula aliwaomba watu kufika katika banda lao lao na hivyo kuweza kupata taarifa juu ya uwepo wa huduma hizo mkombozi kwa maisha yao ya sasa na baadaye.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 


Post a Comment

Previous Post Next Post