Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amezindua boti ya kisasa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5, ambayo itatumika katika shughuli za uokoaji na kuzima moto kwenye Ziwa Nyasa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama wa wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri majini
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amesema ujio wa boti hiyo utasaidia kukabiliana na changamoto za uokoaji majini, majanga ya moto katika vyombo vya usafiri pamoja na upungufu wa vifaa vya kisasa vya uokoaji.
Amesema boti hiyo itaongeza uwezo wa Serikali kuokoa maisha ya wananchi wakati wa dharura, kufika kwa haraka katika maeneo yanayokumbwa na majanga, pamoja na kusaidia katika shughuli za ulinzi na usalama.
Brigedia Jenerali Ahmed pia amesisitiza umuhimu wa kuitunza na kuitumia boti hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akiwataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu za usalama ndani ya maji na kufuatilia taarifa za hali ya hewa kabla ya kufanya shughuli za usafiri majini.
Kwa upande wake, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, amesema Ziwa Nyasa lina mchango mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii, ikiwemo usafirishaji, uvuvi na utalii.
Amesema uwepo wa boti hiyo utaimarisha usalama wa shughuli zinazofanyika katika Ziwa Nyasa na kutoa mazingira salama na ya uhakika kwa wananchi wanaotegemea ziwa hilo kwa shughuli zao za kila siku.
Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma, SSFR Merania Nyabinywino, amesema boti hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 ina injini mbili zenye nguvu ya jumla ya horsepower 500, uwezo wa kubeba mafuta lita 600 na inaweza kubeba abiria 12 kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma, katika kipindi cha Januari hadi Agosti, jeshi hilo limepokea miito 10 ya uokoaji majini na kushughulikia matukio 51 ya moto, yaliyosababisha vifo vya watu saba na majeruhi tisa.
Amesema uwepo wa boti hiyo unatarajiwa kuongeza uwezo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kukabiliana na matukio ya dharura katika Ziwa Nyasa na maeneo mengine ya Mkoa wa Ruvuma, hivyo kusaidia kupunguza vifo na majeraha yanayotokana na ajali na majanga majini.
Kwa upande wao, baadhi ya wawakilishi wa wananchi wameeleza matumaini mapya kutokana na kupatikana kwa boti hiyo, wakisema itaongeza uhakika wa usalama kwa wananchi wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Nyasa pamoja na wageni wanaotembelea maeneo yanayozunguka ziwa hilo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment