NA: MWANDISHI WETU, DODOMA
Wananchi na viongozi wa Zanzibar wamepongezwa kwa kufikia muafaka wa kitaifa kwa kuimarisha umoja na mshikamano kuelekea ujenzi wa taifa lenye maendeleo.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (MCC), Mary Chatanda, Septemba 18, 2026, Jijini Dodoma.
Chatanda amesema, hakuna shaka kuwa, wananchi na viongozi wa Zanzibar, wamesukumwa na dhamira ya dhati ya ujenzi wa taifa lao badala ya kutanguliza tofauti zao za kisiasa na maslahi binafsi.
"Niwapongeze wananchi na viongozi wa Zanzibar ambao waliangalia maendeleo badala ya tofauti zao za vyama, waliangalia Zanzibar waitakayo yenye neema na ustawi badala ya misuguano isiyokwisha, ndiyo maana wakaona wakae pamoja, waelewane ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo," amesema Chatanda.
Aidha, Chatanda amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuwa na hekima, busara na utulivu huku akiwashirikisha kikamilifu viongozi wastaafu na wengine kutoka vyama vya upinzani katika kutafuta muafaka wa pamoja ili Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iundwe na kufanya kazi.
"Rais Dkt. Hussein Mwinyi ameonyesha ukomavu mkubwa wa kiuongozi, kwa kweli nampongeza sana. Vilevile, niwapongeze wanasiasa hasa kutoka Chama cha ACT- Wazalendo, kwa kukubali kukaa meza moja ya mazungumzo ili muafaka upatikane, hatimaye Zanzibar isonge mbele kimaendeleo. Kwa kweli Wazanzibar wamethibitisha kuwa inawezekana kufikia muafaka wa kitaifa kupitia meza ya mazungumzo," amesema.
Ikumbukwe kuwa, tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, kumekuwa na mazungumzo ya pamoja yanayoendelea ili kukamilisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT - Wazalendo.
Septemba 17, 2026, Kamati ya Uongozi ya ACT- Wazalendo, ilikaa kikao maalum kilichofanyika ofisi ndogo za Chama hicho, Vuga Mjini Unguja, ambapo pamoja na mambo mengine, kilifanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kufuatia kikao hicho, Septemba 18, 2026, Rais Dkt. Hussein Mwinyi, alifanya uteuzi wa Othman Masoud Othman, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambapo ataapishwa rasmi Septemba 22, 2026, Ikulu, Zanzibar.
Kukamilika kwa mchakato wa upatikanaji wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kunaendeleza mchakato wa kuteua mawaziri kutoka ACT- Wazalendo ili kukamilisha uundwaji wa serikali ya pamoja ambayo itakuwa chachu ya kuendeleza mipango mizuri ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar huku umoja, amani, upendo na mshikamano ukiwa nguzo kuu ya maendeleo hayo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment