Na. Mwandishi Wetu, DODOMAHalmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea kuboresha Soko la Mnada Mpya lililopo Kata ya Kizota, kwa kufanya ukarabati wa barabara na kuwapangia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara ndani ya soko hilo, hatua inayolenga kuweka mazingira bora na yenye utaratibu.Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Biashara wa Kanda Namba Tatu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma Stephen Maufi alisema kuwa halmashauri imewapangia wafanyabiashara maeneo kulingana na aina ya biashara zao, zikiwemo samaki, matunda na mbogamboga, mishikaki, kuku na viazi. Alisema kuwa zaidi ya wafanyabiashara 150 wamepangiwa maeneo ndani ya soko hilo.Maufi alisema kuwa awali wafanyabiashara wapatao 55 walikuwa wakifanya biashara nje ya eneo la soko, hivyo zoezi hilo limefanyika kuwaingiza ndani ya soko na kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika katika maeneo yaliyotengwa.Alisisitiza kuwa maeneo hayo yametolewa bure kwa ajili ya kufanyia biashara na si kwa ajili ya kupangisha watu wengine. Alisema halmashauri itaendelea kufanya ukaguzi na kuchukua hatua kwa mfanyabiashara atakayepewa eneo lakini asilitumie kwa shughuli iliyokusudiwa.Kwa upande wao, wafanyabiashara waliopewa maeneo walieleza kuridhishwa na zoezi hilo. Alex Hedia, mfanyabiashara wa matunda na mbogamboga,alisema kuwa zoezi limefanyika kwa haki na usawa, huku Mariam Omary, ambaye pia amepangiwa eneo, alisema mpangilio huo utasaidia kuboresha mazingira ya biashara na kurahisisha wananchi kupata huduma.Maboresho ya soko hilo yanaenda sambamba na ukarabati wa barabara katika eneo la soko, huku Halmashauri ikiendelea kusimamia matumizi sahihi ya maeneo yaliyotengwa. Hatua hizo zinalenga kuhakikisha Soko la Mnada Mpya linakuwa na mpangilio mzuri, mazingira bora ya biashara na huduma rahisi kwa wananchi.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment