Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Hasnain Gulamabbas Dewji, ameahidi kuchangia kompyuta, ujenzi wa fremu za maduka pamoja na usambazaji wa maji kwenye vyoo vya Shule ya Msingi Singino, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia shuleni hapo.
Mhe. Dewji ametoa ahadi hizo leo, Septemba 17, 2026, akiwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kuhitimu darasa la saba katika shule hiyo.
Katika ahadi yake ya kwanza, Mbunge huyo amesema atachangia kompyuta kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata msingi wa elimu ya TEHAMA na kuendana na mahitaji ya elimu katika dunia ya kidijitali.
Aidha, ameahidi kuchangia ujenzi wa fremu za maduka zitakazosaidia shule kuwa na chanzo cha mapato, ambayo yanaweza kutumika kukabiliana na baadhi ya mahitaji na changamoto za shule.
Katika eneo la afya na usafi, Mhe. Dewji amesema atasaidia kusambaza maji kwenye vyoo vya shule, hatua inayolenga kuboresha usafi wa mazingira na kusaidia kulinda afya za wanafunzi na jamii ya shule kwa ujumla.
Awali wanafunzi walitoa changamoto hizo kupitia risala yao ilojikita na changamoto hizo na kuomba wasaidiwe ili kuwe na mazingira bora ya kujifunza na kiuchumi
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 2
Post a Comment