Madereva wa Magari madogo ya abiria wametakiwa kufanya matengenezo ya Magari hayo ili kuwaweka abiria wao salama wanapo wasafirisha.
Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika eneo la Ibadakuli barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza ambapo amewaeleza kuwa ubovu wa gari unaweza kusababisha ajali Kwa dereva na abiria aliowabeba wawapo safarini.
Sajenti Ndimila amewasisitiza madereva hao kutii Sheria bila shuruti kwani hatua hiyo itasaidia kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuepukika.
Aidha abiria wameunga mkono elimu hiyo na kuahidi kupaza sauti zao Kwa madereva hao ili kuboresha Magari ya abiria na kusafiri salama.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 2
Post a Comment