" TOENI TAARIFA MUONAPO VITENDO HATARISHI VIKIFANYWA NA DEREVA

TOENI TAARIFA MUONAPO VITENDO HATARISHI VIKIFANYWA NA DEREVA


Abiria wa masafa marefu wametakiwa kupaza sauti zao pindi waonapo vitendo hatarishi vikifanywa na dereva wawapo safarini 

Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Sajenti Ibrahimu Lukumbo katika eneo la Nhelegani barabara ya Shinyanga kuelekea Tinde ambapo amewataka abiria hao kujenga utamaduni wa kutokukaa kimya waonapo vitendo visivyofaa vikitendwa na dereva wa gari Sajenti 

Lukumbo amewaeleza kuwa ni vema kushirikiana Kwa pamoja kuzuia ajali ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza endapo ajali itatokea. Aidha abiria hao wametakiwa pia kutii Sheria bila shuruti ikiwa ni pamoja na kufunga mkanda wa usalama kwenye viti vyao pamoja na kuacha tabia ya kupanda Magari ambayo yamezidi idadi ya abiria wanaotakiwa.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post