Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi amesikiliza kero mbalimbali za kiusalama katika Kata ya Mwasubi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Akizungumza mara baada ya kufika katani hapo SACP Magomi alipata wasaa wa kusikiliza changamoto zinazohusu usalama zilizowasilishwa na wananchi wa Kata hiyo na kuzipatia ufumbuzi.Aidha mkutano huo ulitumika pia kuwapa elimu wananchi hao kuhusu dhana ya Polisi Jamii huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi zinapotokea changamoto zinazowataka kushirikiana na Polisi kama utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu, kutokimbia kutoa ushahidi kwa mashuhuda wa matukio na kuacha tabia ya kuharibu ushahidi ili kukwepa jukumu la kutoa ushahidi mahakamani Aliendelea kuwahimiza kujiepusha na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watu wa jinsia zote na rika zote huku akikazia suala la malezi na kuwataka wazazi kulea watoto wao katika maadili mazuri ya kitanzania ili tuwe na Taifa imara katika siku zijazoMagomi alitumia jukwaa hilo pia kukumbusha wananchi hao kujiandaa na ujio wa mvua za el-nino kama zinavyotabiriwa na mamlaka husika na kuwataka kuchukua tahadhari ili wawe salama. Aliwakumbusha kuzibua mitaro iliyoziba ili kuelekeza maji katika mito na wale wanaoishi mabondeni kuhama kabla mvua hazijaanza kunyesha
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment