RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema tofauti za kiimani zinapaswa kuwa msingi wa kuheshimiana, kuvumiliana na kushirikiana katika kudumisha amani ya Zanzibar.
Dk Mwinyi alisema hayo katika hafla ya kuwekwa wakfu na kumketisha kitini Askofu Lameck Ndomba kuwa askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Zanzibar.
Hafla hiyo ilifanyika kwenye Kanisa Kuu la Kristo, Mkunazini Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi jana.
Dk Mwinyi alisema serikali na taasisi za dini zina wajibu wa kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano, kukuza maadili mema na kuchangia ustawi wa wananchi.
Alisema kanisa na taasisi nyingine za dini zina mchango mkubwa katika elimu, afya, malezi, ujenzi wa maadili na maendeleo ya jamii.
Dk Mwinyi alimpongeza Askofu Lameck Ndomba na kumtakia hekima, afya, nguvu na neema ya Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu ya kuiongoza Dayosisi ya Zanzibar.
Alisema serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya kihistoria kwa lengo la kuhifadhi historia ya Zanzibar, kutoa elimu na kukuza utalii wa kihistoria na kiutamaduni.
Dk Mwinyi alihimiza wananchi wachukue tahadhari na wazingatie taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mvua za vuli zinazotarajiwa kuathiriwa na hali ya El Niño.
Alihimiza taasisi za dini zishirikiane na serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa. Kwa upande wake, Askofu Ndomba alimshukuru Dk Mwinyi kwa ushirikiano anaouonesha kwa taasisi za dini na juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment