Wanafunzi wa Shule ya msingi Negezi iliyopo Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ikiwa ni kuwajengea uelewa wa matumisi sahihi ya barabara ili kujiepusha na ajali za mara Kwa mara.Elimu hiyo imetolewa na Mrakibu msaidizi wa Polisi Zainabu Mangara ambaye ndiye Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga akiambatana na Sajenti Nasoro Mkongowe ambapo wamewaelimisha wanafunzi hao namna sahihi ya uvukaji wa barabara, upande sahihi wa kutembea wakiwa barabarani, ufahamu juu ya alama mbalimbali za barabarani pamoja na namna ya kuepuka michezo hatarishi wakiwa kando ya barabara Mangara amewataka wanafunzi hao pia kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kuwafundisha watoto wengine ambao hawana uelewa kuhusiana na masuala ya usalama barabarani Kwa upende wao Walimu wa Shule hiyo wameipokea elimu hiyo Kwa matokeo chanya kwani wanaamini inaenda kuwa suruhisho la kupunguza ajali za barabarani zinazokuwa zinahusisha wanafunzi katika maeneo yao.PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment