Halmashauri za Wilaya ya Kasulu, ikiwemo Halmashauri ya Mji Kasulu na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, taasisi na wadau mbalimbali wametakiwa kuhakikisha maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño yanafanyika kwa wakati.Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele ambaye amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuzibua mitaro na kuweka sawa mifereji ya maji, kufuatilia maeneo hatarishi na kuwafikishia wananchi taarifa za tahadhari kwa wakati.Akisoma taarifa ya maandalizi ya kukabiliana na El Niño, Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Edwin Laulian amesema Halmashauri imetenga Shilingi milioni 11.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na athari za mvua hizo, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi, kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na kuzibua mitaro na mifereji ya maji.Washiriki wa kikao hicho kutoka taasisi mbalimbali wameeleza kuwa tayari wameweka mikakati ya kukabiliana na athari za mvua hizo kabla, wakati na baada ya kutokea, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano, utayari na utoaji wa taarifa kwa wakati.Mikakati hiyo inalenga kuimarisha utayari wa jamii, kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza, kulinda usalama wa wananchi na mali zao, pamoja na kuhakikisha Wilaya ya Kasulu inakuwa tayari kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









Post a Comment