Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Heche,
amesisitiza umuhimu wa Tanzania kupata Katiba mpya, akieleza kuwa suala hilo ni
muhimu katika kujenga misingi bora ya uongozi na maendeleo ya wananchi.
Heche
ameyasema hayo leo, Septemba 22, 2026, wakati akizungumza katika mkutano wa
hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Jasko, Kata ya Ngokolo,
Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katika
mkutano huo, Heche pia amesisitiza umuhimu wa Serikali kufufua viwanda
vilivyopo nchini ili kuongeza fursa za ajira na kuwawezesha wananchi, hususan
wazawa, kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na uwekezaji na uzalishaji.
Amesema kufufuliwa kwa viwanda kutasaidia kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na maendeleo ya wananchi.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment