Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Pius M. Buzumalle, leo tarehe 23/09/2026 ameongoza kikao cha kawaida cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda.
Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda imefanya kikao chake cha kawaida cha Kamati ya Utekelezaji tarehe 23 Septemba 2026, kikijadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha uhai wa jumuiya, kuongeza ushiriki wa wanachama na kuendeleza miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho, wajumbe walijadili uhai wa Jumuiya ya Wazazi wilayani humo, huku wakisisitiza umuhimu wa wanachama kutekeleza wajibu wao, ikiwemo kulipa ada za uanachama kwa wakati ili kuiwezesha jumuiya kujiendesha na kutekeleza majukumu yake katika ngazi mbalimbali.
Aidha, kikao kilijadili mpango wa kuongeza idadi ya wanachama kupitia elimu na hamasa kwa wananchi na wanachama waliopo, huku Maafisa wa Jumuiya pamoja na Maafisa wa TEHAMA wakipangwa kutembelea matawi na kata kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu namna ya kujiunga na kulipa ada za uanachama kupitia mifumo iliyopo.
Miongoni mwa mambo yaliyopewa uzito katika kikao hicho ni suala la Shule ya Ufundi Misunkumilo, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, ambayo wajumbe walieleza kuwa imekuwa haifanyi kazi kwa zaidi ya miaka mitano.
Kamati hiyo imeeleza umuhimu wa kufanya tathmini ya hali ya shule hiyo, kuboresha miundombinu pamoja na kupanga vizuri eneo lake ili shule hiyo iweze kurejea katika kutoa mafunzo ya ufundi na elimu mbalimbali kwa vijana.
Aidha, kikao kilibaini kuwa eneo la shule hiyo halina hati miliki, hali ambayo imeelezwa kuwa imekuwa ikisababisha sintofahamu kuhusu umiliki wa eneo hilo. Kamati imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha shule hiyo inapata hati miliki kwa ajili ya kulinda mali ya Jumuiya ya Wazazi na kuweka utaratibu mzuri wa matumizi ya eneo hilo.
Wajumbe pia walieleza kuwa changamoto kubwa inayokabili uendelezaji wa shule hiyo si mgogoro na kanisa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali ni pamoja na ukosefu wa fedha kiasi cha Shilingi milioni 2.333 zinazohitajika kwa ajili ya upimaji na upangaji wa eneo, pamoja na umuhimu wa kuwepo mshikamano wa pamoja katika kuendeleza mradi huo.
Kutokana na hali hiyo, Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda imetoa wito kwa wadau mbalimbali wenye nia njema na shule hiyo kujitokeza kusaidia katika hatua za upimaji wa eneo, uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya shule, kwa kushirikiana na viongozi wa Jumuiya pamoja na Chama Cha Mapinduzi.
Katika hatua nyingine, kikao kilijadili umuhimu wa kuanzisha na kuimarisha miradi ya kiuchumi kwa lengo la kuiwezesha Jumuiya ya Wazazi kuwa na uwezo wa kujitegemea kifedha badala ya kutegemea michango pekee.
Wajumbe walihimizwa katika matawi na kata kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo inaweza kuongeza mapato na kusaidia jumuiya kutekeleza shughuli zake, ikiwemo vikao, ziara na shughuli nyingine za maendeleo.
Kikao hicho pia kilipokea taarifa ya tathmini ya maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa, yaliyofanyika katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kuanzia Agosti 27 hadi 29, 2026.
Katika maadhimisho hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Aggrey Mwanri, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, shughuli mbalimbali zilifanyika, ikiwemo mafunzo na mijadala kuhusu malezi, elimu, mazingira, utamaduni na afya, pamoja na michezo mbalimbali kama kuvuta kamba na mpira.
Kushiriki kwa viongozi wa Chama na Serikali katika maadhimisho hayo kulitajwa kuwa sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jumuiya ya Wazazi, Chama Cha Mapinduzi na Serikali.
Kikao hicho kimehitimishwa kwa kusisitiza umuhimu wa viongozi kufanya ziara katika matawi na kata za Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanachama na wananchi kuhusu masuala ya malezi, elimu, mazingira, afya na utamaduni, huku hatua hizo zikilenga kuimarisha uhai na utendaji wa Jumuiya ya Wazazi wilayani humo.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, ameshiriki kikamilifu katika kikao cha kawaida cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mpanda kilichofanyika tarehe 23/09/2026.
Kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa taratibu na miongozo ya Jumuiya, ambapo vikao vya kawaida hufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali na kuimarisha uhai na utendaji wa Jumuiya ndani ya Chama.
Ndg. Heliuth Henry Mbilinyi, maarufu Makete, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Uchumi, Mipango na Fedha kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, ameshiriki katika shughuli za Jumuiya hiyo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment