Halmashauri ya Mji Kasulu imezindua mpango mkakati wa usafi wa mazingira kwa kipindi cha Septemba 2026 hadi 2029, kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa usafi na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira.Mpango huo umezinduliwa katika ukumbi wa mikutano kupitia kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wa Halmashauri, Watendaji wa Kata na Mitaa, Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na wataalamu wa Afya na Mazingira.Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfus Aziz Ndee amewataka Watendaji kutoa elimu kwa wananchi kupitia vikao na kusimamia utekelezaji wa sheria na taratibu za usafi wa mazingira.Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Nduwayo Elias, amewataka watumishi kuwa mfano katika kuhamasisha usafi huku akisisitiza kuzingatia maadili ya utumishi ikiwemo uvaaji wa vitambulisho na mavazi yanayostahili.Watendaji wa Kata na Mitaa, Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na wataalamu wa Afya na Mazingira wameahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kusimamia sheria na kanuni za usafi wa mazingira.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment