Na Mwandishi Wetu, BSKY Media
Waziri mwenye dhamana ya michezo, Paul Christian Makonda, yupo njia panda ya kisheria na kiutendaji kufuatia mkataba wa miaka mitano uliingiwa kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited unaohusu Taifa Stars.
Mashaka hayo yanawekwa bayana wakati Serikali ikiwa imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 6.3 kwa ajili ya Timu za Taifa katika miaka ya hivi karibuni.
Waziri huyo mwenye dhamana na michezo akizungumza na waandishi wa habari leo ameibua maswali mazito 22 yakilenga kuchimbua misingi ya kisheria, kiufundi, na kifedha ya mkataba huo.
Amesema pamoja na TFF kuwa na uhuru wa kiutendaji, Serikali kupitia Wizara na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ina wajibu wa kisheria na kikatiba wa kulinda rasilimali za umma na maslahi ya taifa.
Katika maelezo yake anasema hali ya sintofahamu inaanza tangu ukurasa wa kwanza wa mkataba huo ambao hauna jina mahsusi linalobainisha kwa uwazi kama ni mkataba wa udhamini, usambazaji wa vifaa, au mkataba mseto unaojumuisha mambo yote mawili, licha ya kuhusisha haki kubwa za kibiashara.
Anasema katika Ibara ya 1 na ya 2, mkataba unamtambulisha Sandaland kama "Supplier" wakati huohuo ukimpa ada ya udhamini ya Shilingi bilioni 1.5, vifaa vya Shilingi milioni 300 kwa mwaka, na haki za kipekee za kimatangazo, jambo linaloacha utata mkubwa wa kutenganisha wajibu wake kama mdhamini au msambazaji wa bidhaa.
Aidha Waziri Makonda anasema eneo la ubora na viwango vya vifaa linazua hofu kubwa zaidi . Waziri Makonda anasema wakati Ibara ya 5(6) ikimpa TFF mamlaka ya kuidhinisha miundo na michoro ya jezi (design approval), Waziri anakumbusha kuwa idhini hiyo haimaanishi kuwa bidhaa hiyo imefanyiwa uthibitisho wa kiufundi wa ubora (quality certification). Hali kadhalika, ingawa Ibara ya 5(7) inazungumzia sharti la bidhaa kukidhi "required specifications", mkataba wenyewe hauweki wazi vipimo halisi, aina ya kitambaa, wala chombo kinachopima na kuhalalisha viwango hivyo. Hata katika Kiambatisho Na. II kinachoorodhesha vifaa vya timu za taifa, bei za kila bidhaa (unit prices) hazijajazwa, jambo linalofanya kuwa vigumu kukagua na kuthibitisha kama vifaa vinavyotolewa vinafikia thamani halisi ya Shilingi milioni 300 kwa mwaka kama inavyodaiwa.
Upande wa masuala ya kifedha na kodi nao haupo shwari. Misingi na tathmini (valuation methodology) iliyotumika kufikia kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 haionekani ndani ya mkataba. Vilevile, Ibara ya 5(2) inaweka utata mkubwa wa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) baada ya mwaka wa kwanza bila kuweka wazi nani anabeba mzigo huo, wakati Ibara ya 6 ikichanganya masharti ya malipo kati ya malipo kamili, malipo ya awali ya asilimia 25, na asilimia 50 ya malipo ya mbele. Hata suala la vifaa vya Shilingi milioni 300 linahitaji majibu ya wazi kama vinatolewa bure kama sehemu ya udhamini au vinatakiwa kulipiwa na TFF kupitia mifumo ya "set-off".
Utekelezaji wa mkataba huo pia umeelezwa kukabiliwa na mapungufu ya kiutawala na kisheria. Tarehe ya mwisho ya mkataba inatajwa kuwa ni 31 Juni 2028, tarehe ambayo haipo kwenye kalenda kwa kuwa mwezi Juni una siku 30 tu.
Pia Waziri Makonda amedai nyaraka za mapitio ya utendaji ya kila mwaka (annual reviews) zilizotakiwa kufanyika tangu 2023 hazijawekwa wazi ili kupima kama malipo na usambazaji yalikuwa yakienda sambamba na makubaliano. Aidha, mfumo wa kusitisha mkataba kabla ya muda (Mid-Term Termination) na taratibu za kutotekeleza wajibu (Non-Performance) zimetawanyika katika Ibara tofauti bila uwiano wa kisheria unaolinda maslahi ya pande zote mbili kwa usawa.
Hata hivyo, mapokezi ya kifahari na mambo ya kibiashara yanayoandamana na mikataba ya namna hii yamekuwa yakiibua maswali pia kwa wadau wa michezo, huku baadhi ya wachambuzi wakikumbushia jinsi masuala ya kimkakati yanavyopaswa kuendeshwa kwa umakini mkubwa ili kulinda taswira ya nchi na rasilimali za umma, kama ilivyokuwa ikitokea hata kwenye michakato mingine ya kimataifa ambapo mikataba inatakiwa kuwa wazi na isiyoacha mianya ya upotevu.
Waziri Makonda anahitimisha kwa kuhoji kwa nini kuna juhudi kubwa za kutaka kuaminisha kuwa mkataba huo hauna tatizo wakati nyaraka za mchakato wa ushindani, viwango vya ubora, uthamini wa haki za kibiashara, na ushahidi wa utekelezaji wake haujajibiwa wazi kwa misingi ya kisheria na ushahidi thabiti. Anasisitiza kuwa kuruhusu nyaraka na ushahidi kuzungumza ndiyo njia pekee ya kuthibitisha kama taratibu zote zilifuatwa kwa maslahi mapana ya soka la Tanzani
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment