- Wewe
ni kila kitu kwangu.
- Nitateseka
bila wewe.
- Ninataka
nikwambie tu kuwa ninakuwaza muda wote.
- Ninatamani
kuwa mikononi mwako muda wote.
- Ninakupenda
zaidi ya unavyofikiria.
- Unafanya
mapigo ya moyo wangu yaende mbio nikikuona.
- Najisikia
vizuri mno nikikuwaza mpenzi.
- Ninajihisi
salama nikiwa nawe.
- Nikiwa
mikononi mwako ninajihisi nimefika!
- Ulishaubeba
moyo wangu na sitaki uurudishe.
- Siwezi
kuishi bila wewe mpenzi.
- Sitosahau
usiku ule ambao tuli.
- Tabasamu
lako linanipoteza kabisa.
- Unanistaajabisha
kila siku.
- Nitafanya
lolote ili niwe nawe.
- Ninakutamani
kila saa.
- Ninaona
fahari kuwa na wewe.
- Wewe
ni wangu daima na milele.
- Unanifaa
sana mpenzi.
- Sijui
ningekuwa wapi bila wewe.
- Kila
siku tunapokuwa pamoja naona ninaishi ndoto yangu ya siku nyingi.
- Moyo
wangu unasisimka ninapokuwa nawe.
- Hakuna
mtu aliyewahi kuwa karibu nami na akanifanya nijisikie raha kama
unavyonifanya nijisikie.
- Ninahesabu
muda mpaka pale nitakapo pata busu lako tamu.
- Ni
kama vile uliumbwa kwa ajili yangu.
- Wewe
ni mtu pekee ambaye siko tayari kukuacha.
- Kila
saa wewe ndiye chaguo langu.
- Unanifanya
nijiamini sana mpenzi.
- Wewe
ndiye baraka kubwa niliyowahi kuipata.
- Wewe
ni mzuri sana aisee.
- Nikikuwaza
tu, hata niwe na siku mbaya, itageuka kuwa nzuri tu
- Moyo
wangu unakuhitaji sana sasa.
- Ninatamani
ungekuwepo hapa na mimi.
- Ninavyokupenda
jamani, acha tu!
- Ninajihisi
mwenye bahati sana kukupata wewe kama rafiki wa karibu na mpenzi pia.
- Hata
milele hainitoshi kuwa na wewe.
- Natamani
ungekuwepo hapa ukanishika mkono na ukanivuta kwako.
- Nimekuwaza
siku nzima. Ahsante kwa usiku mzuri kama ule.
- Sikuwahi
kujua kuwa unaweza kummiss mtu hata kabla hajaondoka, mpaka nilipokujua
wewe ndio nikaamini.
- Maisha
yetu pamoja ni tafsiri ya upendo.
- Natumai
uko na siku njema, mwenzio nashindwa kuacha kukuwaza muda wote.
- Daima
hujawahi shindwa kunifanya nitabasamu wakati wote.
- Najikuta
nikishindwa kujizuia kutabasamu kila ninapofikiria kukuona ukirudi toka
kazini.
- Wewe
ni wangu, kipenzi cha nafsi yangu.
- Ninakuthamini
sana mpenzi.
- Unanifanya
nijisikie mwenye bahati sana kuliko wote.
- Natamani
nikupe mabusu mazito kila ninapokuona.
- Nataka
niamke pembeni yako siku zote za maisha yangu.
- Wewe
ni mcheshi sana, unanifanya niwe mwenye furaha wakati wote.
- Ninashukuru
sana nimekujua.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment