Wananchi na wadau mbalimbali katika Mtaa wa Miti Mirefu, Kata ya Mjini, Manispaa ya Shinyanga, wameendelea na juhudi za kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño pamoja na magonjwa ya mlipuko kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Wakizungumza na Misalaba Media Mei 19, 2026, wananchi na wadau hao, wakiwemo Greenheart, Networking Group na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHY COM, wamesema ushirikiano katika kufanya usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi dhidi ya magonjwa ya mlipuko, ikiwemo kipindupindu, kichocho na magonjwa ya ngozi. Wamesema wananchi wa Kata ya Mjini na maeneo mengine ya Manispaa ya Shinyanga wanapaswa kuendelea kutunza mazingira, kusafisha mitaro, kuepuka kutupa taka ovyo na kuacha shughuli zinazoweza kuziba au kuharibu mifereji ya maji. Naye Nassoro Warioba amewataka wananchi na wadau mbalimbali, wakiwemo maafisa usafirishaji, kuwa mabalozi wa usafi katika Mtaa wa Miti Mirefu ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa jamii.PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment