" MWENYEKITI WA CHADEMA AUWAWA NA NG'OMBE – SHINYANGA.

MWENYEKITI WA CHADEMA AUWAWA NA NG'OMBE – SHINYANGA.

Na Mwandishi wetu Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na ng’ombe katika tukio lililotokea Alhamisi, Septemba 3, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea baada ya watu kufika kumchukua ng’ombe huyo nyumbani kwa mzee Mzee Monisa, ambaye alikua mfugaji  kwa ajili ya kwenda kumpandisha jike. 

Inadaiwa kuwa walipomfikia, ng’ombe huyo alikimbia na kufika katika eneo la jirani, anakoishi Mzee Monisa.

Mzee Monisa alichukua fimbo na kujaribu kumrudisha ng’ombe huyo, lakini ng’ombe huyo alimgeukia na kumkanyaga.

Baada ya tukio hilo, Mzee Monisa alikimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

 Inadaiwa kuwa baada ya kufanyiwa vipimo, ilibainika kuwa alikuwa amevunjika mbavu, lakini alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mzee Monisa alikuwa mfugaji, na hadi umauti ulipomkuta alikuwa akihudumu kama Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Ngokolo.

Pia, Mzee Monisa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwinamila, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post