SERIKALI imesisitiza kuwa uwezeshaji wa vijana sambamba na matumizi salama na yenye uwajibikaji ya teknolojia za kidijitali ni nguzo kuu katika kulinda na kuimarisha amani na usalama wa taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Joel Nanauka, alieleza hayo jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, akibainisha kuwa utulivu ndio msingi unaowawezesha vijana kupata elimu, kufanya kazi, kuanzisha biashara, kuonyesha vipaji vyao, na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Waziri Nanauka alionya kuwa matumizi yasiyo na uwajibikaji ya mitandao na teknolojia yanaweza kuchochea usambazaji wa taarifa potofu, lugha za chuki, na migawanyiko, akawahimiza vijana kutumia majukwaa hayo kueneza ujumbe wa matumizi ya kujenga maelewano na mshikamano.
“Tunapowekeza katika vijana, tunawekeza katika amani. Tunapowawezesha vijana kiuchumi, tunaimarisha matumaini,” alisema Nanauka, huku akisisitiza kuwa vijana wenye elimu, ujuzi, na fursa wanayo nafasi thabiti ya kuwa walinzi wa amani na washirika wakuu wa maendeleo.
Katika hatua nyingine, alifichua kuwa serikali kupitia ofisi yake na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, imekamilisha utafiti wa kitaifa kwa ajili ya kuandaa Mkakati wa Taifa wa Vijana, Amani na Usalama. Alieleza kuwa rasimu ya mkakati huo na mpango kazi wake vinalenga kuweka mwongozo wa kitaifa wa kuwawezesha vijana kuzuia migogoro, kukuza mazungumzo, kukabiliana na taarifa za uongo, na kushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment