Mtanzania Nicomed Bohay ameandika historia katika sekta ya fedha barani Afrika baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Pan-Afrika ya EFAfrica Group Ltd (Group CEO), inayojihusisha na ufadhili wa mashine na vifaa vya uzalishaji kwa wakulima, viwanda, biashara, ujenzi na usafirishaji.
Kupitia uteuzi huu, Bohay anaongoza taasisi yenye shughuli zake nchini Tanzania, Kenya, Zambia na Mauritius, akiwa na jukumu la kuongoza mkakati wa kupanua huduma za ukodishaji (leasing) na kuongeza upatikanaji wa vifaa vya uzalishaji kwa maelfu ya wananchi barani humo.
Akizungumzia uteuzi huo, Mwenyekiti Mtendaji wa EFAfrica Group, Dk. Michiel Timmerman, alimuelezea Bohay kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kipekee, nidhamu na dhamira ya kweli ya kuimarisha ujumuishi wa kifedha.
Bohay, ambaye ana uzoefu wa karibu miaka 30 katika sekta ya benki, biashara za kilimo na maendeleo ya ujasiriamali ikiwemo kuongoza PASS Trust na idara ya biashara za kilimo CRDB kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA mwaka 2021, ameweka alama kubwa kupitia usimamizi wa ufadhili wa zaidi ya mashine 4,000 za kilimo nchini Tanzania na kuanzisha mipango ya uwezeshaji kama ile ya ukodishaji wa vifaranga kwa wanawake na vijana, mafanikio yanayoendelea kuipa Tanzania heshima kubwa kimataifa katika uongozi wa taasisi za kifedha.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment