" CCM: Tutaendelea Kuwa Mfano wa Demokrasia na Kuheshimu Mihimili ya Dola

CCM: Tutaendelea Kuwa Mfano wa Demokrasia na Kuheshimu Mihimili ya Dola




Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuwa mfano wa demokrasia nchini huku kikihimiza vyama vingine vya siasa kuiga mfano huo katika uendeshaji wa shughuli zao na uchaguzi wa viongozi.

Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, alipokuwa akifungua mafunzo ya itikadi na uenezi kwa makada wa chama hicho yaliyofanyika katika Chuo cha CCM mkoani Iringa, ambapo alisisitiza kuwa chama hicho kinazingatia misingi ya demokrasia na kuwapa wanachama fursa huru ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Aidha, Wasira alisisitiza kuwa CCM haiwezi kuingilia mihimili mingine ya dola, ikiwemo Mahakama, akieleza kuwa kila mhimili una majukumu yake kikatiba na kwamba kuheshimu mgawanyo wa madaraka na mamlaka yaliyopewa taasisi hizo ni msingi muhimu wa kuendesha nchi kwa kufuata sheria na katiba.

Post a Comment

Previous Post Next Post