Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo, amewasihi vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Kikosi cha 826 KJ Mpwapwa kutokubali kushawishiwa au kulaghaiwa kujiunga na vikundi vya kihalifu, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni usaliti kwa taifa.
Akifunga mafunzo hayo kwa vijana wa kujitolea wa Operesheni Nishati Safi na wa mujibu wa sheria wa Operesheni Linda Amani, Kizigo aliwataka kulinda viapo vyao na kuepuka vitendo vinavyokiuka maadili kama vile matumizi ya dawa za kulevya, huku akiwakumbusha kuwa mafunzo waliyoyapata ya ukakamavu, utii na uzalendo yawafanye kuwa tunu ya kulinda na kulitumikia taifa kwa maslahi mapana.
Katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Brigedia Jenerali Gerald Omar, alifikisha salamu za pongezi kutoka kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda, akiwataka vijana hao kuheshimu yote waliyofundishwa, wakati Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Kanali Ephraim Kituhile, akieleza kuwa mafunzo hayo yanalenga malezi ya vijana, uzalishaji mali na ulinzi wa taifa.
Naye Mkuu wa Kikosi hicho, Luteni Kanali James Michael, alibainisha kuwa pamoja na vijana wengi kujengewa nidhamu na uzalendo, baadhi yao 25 walishindwa kukamilisha mafunzo hayo kutokana na changamoto za nidhamu na afya, huku risala ya wahitimu iliyosomwa na Faraja Noel ikieleza kuwa mafunzo hayo yamewapa maarifa, ujasiri na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment