Mwenyekiti wa umoja wa mkono wafaraja mkoa wa Mbeya Emmanuel Nzunda akizungumza katika hafla ya umoja huo.
Baadhi ya Wanachama wa umoja wa "Mkono wa Faraja", akiwemo Kelvin Mella na Gdeliving Kimaro, wamempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa umoja huo aitwaye Emmanuel Nzunda pamoja na kamati yake kwa maono makubwa ya kuanzisha na kuunda kikundi hicho mkoani Mbeya.
Wanachama hao wameeleza kuwa vikundi vingi vimekuwa vikivurugika kutokana na viongozi kutokuwa wawazi na wakweli, na hivyo wakaomba uongozi huo mpya uwe wa mfano bora ili wafikie malengo yao waliyojiwekea.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa uzinduzi rasmi wa kikundi hicho uliofanyika Septemba 26, 2026, katika Chuo cha Tumaini jijini Mbeya.
Umoja huo umezinduliwa ukiwa na lengo kuu la kusaidia jamii, hasa wenye uhitaji, kuigusa Serikali, pamoja na kufarijiana wanachama wenyewe kwa wenyewe pindi wanapokabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo misiba.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti Emmanuel Nzunda alieleza kuwa alipata wazo la kuanzisha umoja huo ili kujenga mfumo thabiti wa kusaidiana na kupeana faraja katika jamii.
Nzunda alisisitiza kuwa umoja huo utajengwa kwa ushirikiano wa dhati na utakuwa wa faraja pindi mwanachama anapopatwa na msiba, ambapo msiba huo hautakuwa wake peke yake bali utakuwa wa kikundi kizima.
"Changamoto ya msiba ikimpata mtu, hakutakuwa na kuomboleza pekee, bali ni kumfuta machozi mfiwa na umoja huu utajengwa kwa michango na vitendo, wala si maneno," alisema Nzunda.
Kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba Wanachama kuhakikisha wanazingatia masharti ya chama, kushikamana, kusaidiana, kupendana, pamoja na kulipa michango kwa wakati ili kutorudisha nyuma maendeleo ya kikundi.
Aliongeza kuwa kila mwanachama atakiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii na misiba, huku akitangaza kuwa kila mwaka itatolewa sadaka maalum kwa ajili ya kuwatembelea na kuwasaidia wenye uhitaji.
Sehemu ya viongozi hao.Hata hivyo, Nzunda alitoa tahadhari kali kwa wanachama kujiepusha na tabia zinazoweza kubomoa na kusambaratisha umoja huo, zikiwemo,
Usambazaji wa taarifa zisizo na uhakika,
Kejeli, kufokeana kudhalilishana,
Kutoa kauli mbaya na kuleta taharuki
Alisisitiza kuwa tabia hizo ni sumu inayoweza kuua maono mema ya kikundi na kurudisha nyuma maendeleo ya wanachama.
Furaha baada ya kuzindua umoja huo
Hadi sasa, kikundi cha "Mkono wa Faraja" kimefanikiwa kukusanya jumla ya wanachama 543 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na nje ya mkoa huo, ikiwemo Tunduma, Kyela, Mbalizi, Mbarali, Tukuyu, na Chunya.
Kikundi hicho kinaendelea na shughuli zake chini ya kauli mbiu inayosisitiza mshikamano na utu: "Msiba Wako, Msiba Wetu."
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment