" SIHA DC YAFANYA ZIARA DODOMA JIJI KUJIFUNZA UENDESHAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI

SIHA DC YAFANYA ZIARA DODOMA JIJI KUJIFUNZA UENDESHAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI


Na Mwandishi Wetu, DODOMAMadiwani na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Siha wamefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji na usimamizi wa miradi ya kimkakati, ikiwemo ushirikishwaji wa wadau na wawekezaji katika utekelezaji wa miradi hiyo.Ziara hiyo imepokelewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, ambaye amewataka viongozi na wataalam hao kutumia uzoefu walioupata Dodoma katika kuboresha utekelezaji wa miradi katika halmashauri yao, pamoja na kuwashirikisha wawekezaji tangu hatua za awali za maandalizi ya miradi.“Elimu mtakayoipata hapa mkaiboreshe na kufanya kwa ukubwa zaidi kwenu. Kama miradi yenu itahusisha wawekezaji, washirikisheni tangu mwanzo ili kuhakikisha mnafanya miradi hiyo kwa ubora zaidi,” alisema Mstahiki Meya Chaula.Aidha, iliwasilishwa taarifa kuhusu uendeshaji wa miradi miwili ya kimkakati inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ni Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma na Hoteli ya Jiji.Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Stanley Nkini, aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mapokezi mazuri pamoja na elimu waliyopatiwa, akisema kuwa uzoefu walioupata utawasaidia katika utekelezaji wa miradi yao, hususan mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi.“Tumeona tuje Jiji la Dodoma kujifunza kwa sababu wana kituo kikubwa na kizuri cha mabasi. Mazuri tunayoyaona hapa Dodoma tutayapeleka Siha” alisema Nkini.Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Marco Masue, alisema kuwa ziara hiyo imewapa fursa ya kujifunza na kujionea namna miradi mbalimbali inavyotekelezwa, ukiwemo mradi wa Hoteli ya Jiji la Dodoma wenye ghorofa kumi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post