Na Mapuli Misalaba
Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewahimiza wanachama kutumia mifumo ya
kidijitali kuhakiki taarifa za michango na mafao yao mapema ili kubaini makosa
na kuepuka changamoto wakati wa kudai mafao.
Wito huo
umetolewa leo, Septemba 18, 2026, mjini Shinyanga wakati wa semina ya PSSSF kwa
waandishi wa habari kutoka Klabu za Waandishi wa Habari za Shinyanga na Simiyu
pamoja na Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN).
Akizungumza
katika semina hiyo, Afisa Msimamizi wa PSSSF Mkoa wa Simiyu, Salum Mwegelo,
amesema wanachama wanapaswa kufuatilia taarifa zao mara kwa mara badala ya
kusubiri hadi wanapokaribia kustaafu.
Aidha,
Mwegelo amewataka wastaafu kuwa makini na watu wanaojitambulisha kama mawakala
wa PSSSF, akisisitiza kuwa mfuko huo hauna mawakala wanaotoa huduma kwa niaba
yake.
Amesema
wastaafu wanapaswa kutumia njia rasmi za PSSSF na kutotoa taarifa za siri,
ikiwemo namba za siri za akaunti zao, kwa watu wasiokuwa na mamlaka.
Kwa upande
wake, Kaimu Afisa Mfawidhi PSSSF Shinyanga, Sunday Rashid, amesema mfuko
umeanza kushughulikia taarifa za watumishi wanaokaribia kustaafu miezi sita
kabla ya tarehe yao rasmi ya kustaafu ili kutoa muda wa kuhakiki taarifa na
kurekebisha changamoto.
Naye Mratibu
wa TBN Kanda ya Ziwa, Kadama Malunde, amewasisitiza waandishi wa habari kutumia
taaluma yao kuwafikishia wananchi elimu sahihi kuhusu haki, wajibu na huduma za
hifadhi ya jamii.
Amesema waandishi na wanablogu wana wajibu wa kuhakikisha taarifa wanazozifikisha kwa umma zinathibitishwa, zina usahihi na zina manufaa kwa jamii.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment