" BAKWATA YATOA WITO WA KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO NA KUKEMEA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII

BAKWATA YATOA WITO WA KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO NA KUKEMEA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII




Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetoa mwito kwa viongozi na waumini wa Kiislamu kutumia mafundisho ya dini kuchochea upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi na kuondoa utamaduni wa kuombaomba.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma, Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Dk Abubakar Zubeir, amesema mkoa huo ni kitovu cha mafundisho ya dini na eneo la kimkakati kiuchumi na kibiashara, hivyo viongozi wanapaswa kuandaa maandiko ya miradi na kuomba ardhi ya kutosha.

Aidha, kufuatia kukamilika kwa uchaguzi mkuu na uchaguzi wa ndani wa Bakwata, Mufti Zubeir amewataka viongozi na waumini kuacha malumbano yote na badala yake kujikita katika kushirikiana kuleta maendeleo nchi nzima.

Katika hatua nyingine, Mufti Zubeir amekemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayofanywa na baadhi ya vijana kuwatukana viongozi na kuhatarisha amani, akisisitiza kuwa teknolojia hiyo inapaswa kutumika kwa tija ikiwemo matumizi ya akili unde ili kuchochea maendeleo badala ya kuchochea machafuko.

Post a Comment

Previous Post Next Post