" MWENYEKITI WA WAZAZI CCM: WAHARAKATI NA WANASIAZA WANAWEZA KUCHELEWESHA KATIBA MPYA

MWENYEKITI WA WAZAZI CCM: WAHARAKATI NA WANASIAZA WANAWEZA KUCHELEWESHA KATIBA MPYA




Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhil Maganya, amesema baadhi ya kauli na matendo yanayotolewa na wanasiasa na wanaharakati yana uwezekano mkubwa wa kuchelewesha upatikanaji wa Katiba mpya nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma mkoani Mara, Maganya ameiomba Serikali kuendelea na mchakato huo kwa kuzingatia misingi ya maridhiano, akisisitiza kuwa suala la Katiba ni la Watanzania wote na halipaswi kuamuliwa au kuendeshwa na kundi moja pekee.

Maganya amefafanua kuwa baadhi ya wanasiasa wanajaribu kuhodhi mchakato huo kwa kuweka masharti, huku wakisahau kuwa nchi ina vyama vya siasa 19 vyenye usajili wa kudumu na jumla ya wananchi zaidi ya milioni 61.

Amewataka viongozi hao na wanaharakati kuacha kauli na matendo yanayoweza kuyumbisha nchi, na badala yake kutoa fursa kwa wananchi kuwa na subira wakati Serikali ikifuata ratiba iliyowekwa ya kufikia maridhiano kabla ya kuendelea na hatua za mchakato wenyewe.

Aidha, ametoa wito maalum kwa wananchi kutosikiliza kauli za watu wanaochochea mgawanyiko na badala yake kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kusimamia mchakato wa Katiba mpya kwa amani. Kupitia msimamo wake, ameiomba Serikali kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuleta sintofahamu na badala yake kuelekeza nguvu kwenye jambo hilo ambalo Watanzania wengi wanalisubiri kwa hamu kubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post