Serikali imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia, hususan akili unde na ubunifu, ili kukuza sekta ya utalii na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii la kimataifa.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Ashatu Kijaji, wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka mnamo Septemba 27, ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu inayosisitiza umuhimu wa teknolojia katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta hiyo.
Dk. Kijaji alibainisha kuwa matumizi ya teknolojia yana mchango mkubwa katika kuboresha huduma za utalii, kuimarisha uuzaji na utangazaji wa vivutio, pamoja na kuongeza ushindani wa nchi kimataifa.
Alisema kuwa uwekezaji unaochochea mageuzi ya teknolojia, uchumi, ubunifu na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) umesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha msimamo wa Tanzania katika soko la kimataifa la kitalii.
Aidha, Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika nyanja za uwekezaji, utoaji wa huduma za utalii, uendelezaji wa miundombinu, kuibua mazao mapya ya utalii, kuimarisha uhifadhi wa maliasili na malikale, pamoja na kutangaza vivutio mbalimbali vya nchi.
Aidha Waziri Kijaji aliwahimiza wadau wote wa utalii kuimarisha ushirikiano na kuwekeza kikamilifu katika teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha utalii unanufaisha jamii, unalinda rasilimali zilizopo, na unachangia katika maendeleo endelevu ya taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 03
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment