" Waandishi wahimizwa kupanua wigo wa habari

Top News

Waandishi wahimizwa kupanua wigo wa habari




Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Habari, Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari kupanua wigo wa habari wanazoripoti kwa kuangazia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, badala ya kujikita zaidi katika michezo na burudani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Clouds Media Group waliokuwa wakishiriki mafunzo kwa siku tano kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba, 2026 kuhusu mchakato na taratibu za ithibati, Bw. Mhando amesema pamoja na umuhimu wa habari za michezo na burudani, vyombo vya habari vina wajibu wa kuibua na kuripoti masuala mengine yenye maslahi kwa Taifa.

“Ni sawa kuzungumzia michezo, lakini isiwe wakati wote. Lazima sisi kama Waandishi wa Habari tuone na kuripoti mambo mengine yanayoendelea katika nchi yetu,” amesema Bw. Mhando.

Amesema Waandishi wa Habari wa ndani wana haki na wajibu wa kuripoti matukio yanayotokea nchini kwa usahihi na kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, badala ya kuacha simulizi kuhusu Tanzania zijengwe na Waandishi wa Habari kutoka nje ya nchi kwa namna inayoweza kuathiri taswira yake.

“Waandishi wa Habari wana haki ya kuripoti mambo yanayotokea nchini mwetu bila kusubiri Waandishi wa Habari kutoka nje, ambao wanaweza kuripoti kwa namna inayoharibu taswira ya nchi. Waandishi wa Habari wa ndani wakiripoti kwa usahihi, wanaweza kulinda heshima ya nchi na kusaidia utekelezaji wa mipango yake,” amesema.

Aidha, Bw. Mhando amesisitiza umuhimu wa Waandishi wa Habari kufahamu taratibu za ithibati na kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni, ili taaluma ya uandishi wa habari itekelezwe kwa weledi na uwajibikaji.

Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa kuhusu mchakato wa ithibati, vigezo vinavyotumika na umuhimu wa kuwa na nyaraka pamoja na taarifa zinazohitajika wakati wa kuomba ithibati.

JAB imeendelea kushirikiana na vyombo vya habari na kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kuongeza uelewa kuhusu taratibu za ithibati na wajibu wa Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa majukumu yao.Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa za uwekezaji kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post