" Mkopo wa BoT wachagiza mauzo ya mazao nje

Mkopo wa BoT wachagiza mauzo ya mazao nje




BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema mkopo wa Sh trilioni moja uliotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa benki za biashara, umeongeza kiwango cha mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege amesema mauzo hayo yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.2 hadi Dola za Marekani bilioni 3.5 na yanatarajiwa kufika Dola za Marekani bilioni tano ifikapo mwaka 2030.

Nyabundege alisema hayo jijini Arusha alipozungumza kwenye Kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds cha Kampuni ya Clouds Media jana asubuhi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita iliielekeza BoT izikopeshe benki za biashara Sh trilioni moja kwa riba ya asilimia tatu ili ziwakopeshe wakulima kwa riba ya chini ya asilimia 10.

Kwa mujibu wa Nyabundege, wakulima wamekuwa wakipatiwa mikopo yenye riba nafuu iliyowezesha taifa kujitosheleza chakula kwa asilimia 130.

Alisema katika miaka mitano ili“Tuna uwezo wa kuzalisha chakula chetu kwa asilimia 100 na tukawa na uwezo wa kuwauzia majirani zetu asilimia 30 iliyobaki, wapo badhi ya majirani zetu hata kufikia asilimia 80 ya mahitaji ya chakula chao hawafikishi,” alisema Nyabundege.

Alisema katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 TADB imeendelea kutoa mikopo na mitaji kwa wakulima vijana na akina mama. Nyabundege alisema mikopo iliyotolewa katika sekta ya kilimo mwaka 2021 ilikuwa ni “Tunatoa dhamana kwa vijana na akina mama ambayo tunaiita smaller holder guarantee scheme (dhamana kwa wakulima wadogo wadogo) kupitia benki 20 nchini… Watu wasiokuwa na dhamana wakienda kwenye benki hizo wanapewa mikopo na TADB inawapa dhamana,” alisema Nyabundege.

Aliongeza: “Zamani watu walikuwa wanafikiria sekta ya kilimo ni sekta hatarishi, benki ziliacha kutoa mikopo, sisi Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB tuliwaambia hapana, kilimo ‘kina-benkika’ na ndo slogan (kaulimbiu) yetu”.

Post a Comment

Previous Post Next Post