Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu amepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wananchi.
Mhe. Sangu ametoa pongezi hizo Septemba 13, 2026 wakati akizundua mradi wa nishati safi ya kupikia katika shule ya Sekondari ya Kinambeu iliyopo wilaya ya Iramba, Mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhana ya kurejesha kwa Jamii (Corporate Social Responsibility) iliyofadhiliwa na WCF.
Aidha, amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira, kupunguza athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati chafu na kuboresha maisha ya wananchi.
Amesema, Dira ya Taifa ya 2050 kupitia nguzo namba 3 inasisitiza kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi.


“Nikupongeze Mkurugenzi Mkuu wa WCF kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kutekeleza kwa vitendo vipaumbele vya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 kwa kuwezesha jamii ya wanairamba majiko yanayotumia nishati safi.,” amesema
Kadhalika, Waziri Sangu amewataka Viongozi wa Halmashauri, Walimu pamoja na Wanafunzi kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo ya Nishati Safi ili uwekezaji huo pia uweze kutumiwa na vizazi vijavyo vya wanafunzi watakaokuja kusoma katika shule hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Mwenda ameishukuru Serikali kwa kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo sekta ya elimu, afya, miundombinu, nishati ya umeme na maji.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma amesema mradi huo wa nishati safi umesaidia takribani wanafunzi 2,000 wanaosoma katika shule ya sekondari ya Kinambeu na Kizaga zilipo katika halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Amesema, msaada huo umelenga kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo inaenda sambamba na utunzaji wa mazingira ambapo kiasi cha shilingi Milioni 40 zimetumika kusimika miundombinu ya nishati safi ya kupikia.
Kwa upande wake Kaka Mkuu wa shule ya Sekondari Kinambeu Mikidadi Lyanga anayeoma kidato cha tano alishukuru WCF kwa kuweka miundombinu bora ya nishati safi ya kupikia ambapo alieza manufaa yake kuwa ni kusaidia chakula kupikwa kwa muda mfupi na kusaidia utunzaji mazingira ambapo kuni hazitatumika tena.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment