" Zanzibar wadhamiria 100,000 kuwa na faiba

Zanzibar wadhamiria 100,000 kuwa na faiba




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema Serikali inalenga kuunganisha kaya 100,000 na huduma ya intaneti kupitia mfumo wa Fibre-to-the-Home ndani ya miaka mitatu.

Amesema Serikali pia inaandaa Mfumo Mkakati wa Akili Unde utakaotoa mwongozo wa matumizi salama na yenye uwajibikaji ya teknolojia hiyo.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, Septemba 29, 2026, wakati akifungua Maonesho ya Teknolojia na Akili Unde (Tech and AI Expo Zanzibar 2026) katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar, sambamba na uzinduzi wa Sera ya Kidijitali ya Zanzibar 2026.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti kuendeleza mageuzi ya kidijitali kwa kuimarisha miundombinu, kuongeza matumizi ya teknolojia katika huduma za umma na uchumi, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wabunifu na wawekezaji.

Katika hafla hiyo, Dkt. Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati (MoU) kati ya Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar na Huawei Technologies Tanzania Limited.

Post a Comment

Previous Post Next Post