Madereva wa bajaji za mizigo katika eneo la Bijampola Manispaa ya Kahama wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusiana na umuhimu wa kuzingatia Sheria ya usalama barabarani na kutii Sheria hiyo bila shuruti.Elimu hiyo imetolewa na Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Kahama Mrakibu wa Polisi Frola Nangawe akiambatana na Askari wa Kikosi hicho Sajenti Nuran Mwakitubu na Sajenti Balbina Donge ikiwa ni sehemu ya operesheni za Kikosi Cha usalama barabarani katika kuzuia makosa hatarishi na ajali zinazoweza kuepukika.Mrakibu wa Polisi Nangawe amewataka madereva hao kuacha kupakia mizigo na abiria pamoja lakini pia kuepuka kubeba mizigo Kwa njia hatarishi akisisitiza kuwa vitendo hivyo vimekuwa sehemu ya visababishi vya ajali za mara Kwa mara barabarani.Aidha amewaeleza kuwa utii wa Sheria bila shuruti huepusha ajali zisizo za lazima na kuimarisha usalama Kwa watumiaji wote wa barabara.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment