Mashindano ya mchezo wa Bao yaliyoandaliwa na Mwl. Silvester Sugwejo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Kasulu kwa lengo la kuenzi kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yamehitimishwa rasmi kwa kuwapata washindi wa nafasi tatu za juu.Huya Sinde, maarufu kwa jina la Bubu kutoka Kijiwe cha Kimobwa ameibuka mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Jeremiah Jenks kutoka Kijiwe cha Mtanzania aliyeshika nafasi ya pili, huku Musa Nkulangowe kutoka Mnadani akishika nafasi ya tatu.Akizungumza baada ya mashindano hayo, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Venatus Edward amewahimiza wachezaji kuunda vikundi katika vijiwe vyao na kusajili wanachama ili vitambulike rasmi na kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.Kwa upande wake, mdhamini wa mashindano hayo, Mwalimu Silvester Sugwejo ameahidi kuendelea kushirikiana na wachezaji kutoka vijiwe mbalimbali kwa kudhamini mashindano yatakayowakutanisha wadau wa mchezo huo.Naye Diwani wa Kata ya Murubona, Jumanne Mustapha amewapongeza washiriki na kuhimiza kuendelezwa kwa mchezo wa Bao kama sehemu ya kuhifadhi na kuenzi utamaduni wa Mtanzania.Mashindano hayo yamefanyika kwa siku mbili na kuwakutanisha washiriki 21 kutoka vijiwe mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Mji Kasulu.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



















Post a Comment