Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yamefanyika Oktoba 16, 2026, Wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma, yakilenga kuihamasisha jamii kutokomeza ukatili wa kijinsia na kulinda haki za mtoto wa kike.Maadhimisho hayo, yamefadhiliwa na shirika la Plan International kupitia Mradi wa Wezesha Binti ambayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari Bogwe.Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya, mgeni rasmi Huruma Andrew Mushi amewataka Watendaji kuhakikisha kamati za kupinga ukatili zinafanya kazi ipasavyo na kuitaka jamii kuacha kuwaozesha watoto katika umri mdogo na kuwakinga dhidi ya mimba za utotoni.Kwa pande wake, Mratibu wa Mradi wa Wezesha Binti, Sifumungu Lazaro Exavery, amesema mradi huo unalenga kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali, Dini, Kimila na jamii kwa ujumla.Aidha, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Kasulu, Inspekta Maimuna Abdul Omari amesisitiza kuwa wataendelea kusimamia sheria na kuhakikisha watuhumiwa wa ukatili wanachukuliwa hatua za kisheria.Katika hatua nyingine, Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Thobieta Adrian Kasuga amewahimiza walimu kuwa karibu na wanafunzi,kuwasikiliza na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili.Hata hivyo, Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Maendeleo ya Jamii wameahidi kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto.Katika hatua nyingine, Watoto wameiomba jamii kuepuka mila na desturi zenye madhara na kuimarisha mawasiliano kati ya wazazi na walimu ili kuhakikisha usalama wao.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 06🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254























Post a Comment