Wafanyabiashara wa nyama Halmashauri ya Mji Kasulu, Mkoani Kigoma, wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Bodi ya nyama ili kuhakikisha nyama zinazouzwa zinakuwa bora na salama kwa afya za watumiaji.Wito huo umetolewa na Msimamizi wa Bodi ya nyama Kanda ya Magharibi, Abdallah Waziri alipotembelea machinjio ya nguruwe yaliyopo Mtaa wa Busokelo, Kata ya Nyansha na kubainisha kuwa kila anayejihusisha na shughuli za nyama wakiwemo wachinjaji na wauzaji wanapaswa kutambuliwa na Bodi ya nyama na kutimiza masharti yanayotakiwa.Amesema hatamvumilia mtu yeyote anayefanya biashara ya nyama kinyume cha sheria akisisitiza kuwa lengo ni kuwaondoa wasio na sifa na kuhakikisha shughuli hizo zinafanywa na watu wanaokidhi vigezo vilivyowekwa.Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Sabinus Chaula amewataka wafanyabiashara kushirikiana na Mamlaka husika kutoa taarifa sahihi kuhusu ukiukwaji wa taratibu, hususan uuzaji wa nyama za mifugo iliyokufa na uchinjaji usiofuata kanuni.Amesisitiza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kulinda afya za wananchi na mapato ya Serikali kwa kutoa taarifa za vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nyama.Naye Katibu Tarafa wa Tarafa ya Heru chini , Hassan Lucas amesema ukaguzi wa bucha na maeneo ya uchomaji nyama ni zoezi endelevu, hivyo operesheni zitaendelea hata baada ya wataalamu kukamilisha ziara yao, kwa lengo la kuhakikisha wafanyabiashara wote wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


















Post a Comment