Halmashauri ya Mji Kasulu imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa huduma za afya kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha tathmini ya huduma za afya Mkoa wa Kigoma, kilichofanyika tarehe 16 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Kasulu Motel. Kikao hicho kimewakutanisha Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya Mkoa (RHMT) na Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya za Halmashauri zote nane za Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa huduma hizo na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.Akizungumza katika kikao hicho, Mgeni Rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma ambaye Hamza S. Mnaliwa amezitaka RHMT, CHMT na wadau wa sekta ya afya kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya afya. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuoanisha taarifa zinazowasilishwa na changamoto zilizobainishwa pamoja na hatua zinazochukuliwa kuzitatua, huku akihimiza matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa taarifa na utekelezaji wa maazimio ya kikao.Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Damas J. Kayera amewataka washiriki kushiriki kikamilifu katika majadiliano na kutoa michango yenye tija itakayosaidia kuboresha huduma za afya katika Halmashauri husika na Mkoa kwa ujumla.Kikao hicho cha siku mbili kinalenga kutathmini utekelezaji wa huduma za afya kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza. Ushiriki wa Halmashauri ya Mji Kasulu ni sehemu ya jitihada za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment