" MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA KUPOZA UMEME WA MALANGALI – RUKWA

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA KUPOZA UMEME WA MALANGALI – RUKWA

 Rukwa:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amekagua Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 na Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Malangali Sumbawanga.

 Ndejembi amekagua mradi huo katika mtaa wa mji mwema kata ya Malangali manispaa ya Sumbawanga ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 400 kutoka Tagamenda, Iringa hadi Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, pamoja na ujenzi wa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha msongo wa Kilovoti 400/220/66/33, Maangali, Sumbawanga.

Wakati akikagua mradi huo, Makamu wa Rais alipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme Tanzania ( TANESCO) Lazaro Twange kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na kuridhishwa na kasi ya kazi inayoendelea.

Amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya nishati ili kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika, wa kutosha na wenye ubora, ili kuchochea maendeleo ya viwanda, biashara na uchumi wa wananchi.

Twange amesema Mradi huu ni sehemu ya Mradi wa Kuunganisha Gridi ya Umeme kati ya Tanzania na Zambia (TAZA), unaolenga kuunganisha mifumo ya umeme ya nchi hizo mbili ili kuwezesha biashara ya umeme kikanda, kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Naye Emanuel Stanslaus, mkazi wa Sumbawanga, amesema mradi huo utafungua fursa za uwekezaji na ajira kwa vijana.

“Mradi huu utawavutia wawekezaji kuja Sumbawanga. Kama wananchi tuko tayari kuutunza na kushirikiana na TANESCO,” amesema Emanuel .

Kwa mujibu wa Twange mradi huo ambao umefikia asilimia 92 umegharimu zaidi ya sh Tri.2 kwa vituo vyote vitano vya Tagamenda ,Iganzo ,Mafinga,Nkangamo na Malangali na upo katika hatua za mwisho.  

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 09

 

Post a Comment

Previous Post Next Post