Na Lydia Lugakila Misalaba Media Mbeya:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe, Deogratius John Ndejembi, ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya njia nne ya TANZAM yenye urefu wa kilomita 29. Mradi huo unagharimu Shilingi bilioni 183.708, ambapo tayari mkandarasi amepokea malipo ya Shilingi bilioni 40.Akiwa eneo la Kabwe baada ya ziara ya kukagua mradi huo pamoja na miradi ya umeme na maji mnamo Oktoba 16, 2026, Makamu wa Rais amekemea kitendo cha mkandarasi kutindua barabara na kufunga mitaa bila maandalizi thabiti hatua inayosababisha adha ya vumbi pamoja na kukwamisha shughuli za usafiri na biashara jijini humo.Kufuatia hali hiyo, Makamu wa Rais amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, kuhakikisha kuwa barabara zote za mitaa zilizofungwa zinafunguliwa huku maeneo ya katikati ya jiji kama vile Mwanjelwa yakipewa kipaumbele cha kwanza. Kwa upande wake waziri wa Ujenzi amebainisha kuwa atahakikisha anasimamia kwa kazi hiyo kwa hali na mali ili kuwaondolea wananchi changamoto hiyo.Aidha Mhe Ndejembi amesema kuwa Serikali haitavumilia hali hiyo ya kuona mradi ahuo ukisuasua tena .Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, ameeleza kuwa barabara hiyo itakapokamilika itakuwa na madaraja pamoja na vivuko vya watembea kwa miguu (vya juu na chini) katika maeneo ya Kabwe, Mwanjelwa, Uyole, na Mbalizi.Hata hivyo, Spika Mstaafu, Dkt. Tulia Ackson, aliwashukuru watendaji wa TANROADS Mkoa wa Mbeya kwa utayari wao wa kuitika na kutatua changamoto za miundombinu ya barabara mkoani humo.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment