" MAPOKEZI YA KAIMU KATIBU WA CCM MKOA WA KATAVI YAFANYIKA, ASISITIZA UMOJA, UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU YA KAZI

MAPOKEZI YA KAIMU KATIBU WA CCM MKOA WA KATAVI YAFANYIKA, ASISITIZA UMOJA, UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU YA KAZI

KAIMU Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Ndugu Hawa Siri Makonyola, amesisitiza umuhimu wa viongozi, watendaji na wanachama wa chama kuwa na umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao na kukijenga chama.

Ndugu Hawa Siri ametoa msisitizo huo wakati akizungumza katika tukio la mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Katavi, ambapo ameeleza kuwa umoja na mshikamano ni muhimu katika kuhakikisha shughuli za chama zinaendelea kutekelezwa kwa ufanisi.

Amesema kila kiongozi na mtendaji anapaswa kutambua nafasi yake na kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, upendo na amani, huku akiwataka viongozi na wanachama kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama.

Aidha, Kaimu Katibu huyo amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhai wa CCM na jumuiya zake kwa kuendelea kusajili wanachama wapya pamoja na kuhamasisha wanachama waliopo kutekeleza wajibu wao wa kulipa ada za chama.

Amesema juhudi za kukijenga chama zinapaswa kuanzia katika kuhakikisha wanachama wanaongezeka na jumuiya za chama zinaendelea kuwa hai, huku viongozi na watendaji wakibeba wajibu wa kuhamasisha wanachama kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama.

Katika hatua nyingine, Ndugu Hawa Siri amesisitiza nidhamu ya kazi kuwa sehemu muhimu ya utendaji wa viongozi na watendaji, akiwataka kuzingatia weledi, uwajibikaji na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema nidhamu katika kazi ni muhimu katika kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia taratibu na misingi ya utendaji wa chama.

Ndugu Hawa Siri Makonyola amesisitiza pia umuhimu wa upendo na amani katika utekelezaji wa majukumu, akiwataka viongozi na wanachama kudumisha mahusiano mazuri, kuheshimiana na kushirikiana katika kukijenga Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi.

Mapokezi ya Kaimu Katibu huyo yamefanyika tarehe 02 Oktoba 2026 katika Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Katavi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kumkaribisha katika nafasi hiyo na kuendelea na majukumu ya chama mkoani humo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Ndug. Iddi Hassani Kimanta, ameongoza kikao cha mapokezi ya Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndug. Hawa Siri Makonyola, yaliyofanyika leo tarehe 02/10/2026.

Mapokezi hayo yamejumuisha viongozi wa CCM Mkoa wa Katavi, Sekretarieti ya Mkoa pamoja na viongozi wa chama kutoka ngazi ya Wilaya.

Ndug. Pendo Machimu, Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi (UVCCM),  tarehe 02/10/2026, amesalimia na kujitambulisha kwa viongozi wakati wa mapokezi ya Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndug. Hawa Siri Makonyola.

Ndug. Pendo Machimu ameshiriki kikamilifu katika mapokezi hayo yaliyofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Katavi.




PROFESSOR MGOKO EPISODE 04

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post