Mdau wa elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa The BSL Investments Company Limited, Peter Frank Lugumi maarufu kama Mr. Black, amekabidhi vifaa vya michezo kwa shule nne za msingi katika Manispaa ya Shinyanga kupitia mpango wake wa kijamii wa Box la Faraja.Katika zoezi hilo, Mr. Black ametoa seti nne za jezi kwa shule za msingi za Uzogore, Negezi, Mwamashele na Hochwalt, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha ushiriki wa wanafunzi katika michezo na kukuza vipaji mashuleni.Shule zilizofaidika na msaada huo ni:- Shule ya Msingi Uzogore – Ibadakuli- Shule ya Msingi Negezi – Mwawaza- Shule ya Msingi Mwamashele – Kizumbi- Shule ya Msingi Hochwalt – IbinzamataMbali na vifaa vya michezo, Mr. Black ameelekeza nguvu katika mahitaji mengine ya msingi ya shule hizo. Katika Shule ya Msingi Uzogore, amechangia ukarabati wa majengo pamoja na kutoa viti kwa ajili ya walimu.Katika Shule ya Msingi Negezi, ametoa fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa mapipa ya kuhifadhia maji, hatua inayolenga kusaidia kuboresha mazingira ya shule na upatikanaji wa maji kwa matumizi ya wanafunzi na walimu.Aidha, Mr. Black ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa ukuta wa Shule ya Msingi Jomu, akiongeza nguvu katika jitihada za kuboresha usalama na mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.Msaada huo ni sehemu ya mwendelezo wa mpango wa Box la Faraja, unaolenga kuchangia maendeleo ya shule kupitia kuboresha miundombinu ya elimu, michezo na mazingira ya kujifunzia katika Manispaa ya Shinyanga.Akizungumza kuhusu mpango huo, Mr. Black amesisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana na taasisi za elimu ili kuhakikisha changamoto zinazokabili shule zinapata nguvu ya pamoja katika kutatuliwa.Ameahidi kuendelea kushikamana na taasisi za elimu na wadau wengine wa maendeleo katika kusukuma mbele jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia, kukuza vipaji vya wanafunzi na kuimarisha ubora wa elimu katika Manispaa ya Shinyanga.Box la Faraja — Tunagusa Elimu, Tunajenga Mazingira, Tunakuza Vipaji.




🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




























Post a Comment