Wazazi na walezi wanahimizwa kuwalea watoto katika mazingira salama, yenye upendo, heshima na mawasiliano mazuri, pamoja na kuwafundisha kutambua vitendo vya ukatili na unyanyasaji. 

Wito huo umetolewa na Polisi wa Kata ya Ikoma Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Emmanuel Kisiri alipotembelea familia ya Thomas Thomas wa Kijiji cha Parknyigoti.

Amesema kuwa ulinzi wa mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji huanzia nyumbani kupitia malezi bora yanayotolewa na wazazi na walezi hivyo watoto wanapaswa kupewa nafasi ya kueleza changamoto zinazowakabili bila hofu, ili iwe rahisi kwa wazazi na walezi kubaini mapema viashiria vya ukatili na kuchukua hatua zinazofaa.

Jamii inakumbushwa kuwa malezi bora si jukumu la mzazi pekee, bali ni wajibu wa jamii nzima kuhakikisha kila mtoto anakua katika mazingira yenye usalama, haki na upendo.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 06


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254