Na.Mwandishi wetuMwanzaMfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imeanza kutekeleza rasmi huduma nne mpya za kuboresha ustawi wa watumishi na wastaafu, hatua inayotekeleza maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kusikiliza na kutatua kero za wastaafu.Hayo yamesemwa na Bwana Venant William , Afisa Matekelezo Mkuu, Kanda ya Ziwa ambapo amebainiaha kuwa,huduma hizo zimeanza kutumika rasmi Januari 1, 2025 kufuatia tangazo lililotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete, januari mwaka jana.Bwana William amefafanua wakati akiwasilisha mada katika kongamano la wahariri liliyofanyika Oktoba 12, 2026.kongamano hilo lililenga kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi za umma, lililoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), "Huduma hizo ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha chini cha pensheni ya mwezi kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 20,0000. Hatua hii inalenga kumuinua mstaafu wa kipato cha chini kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha".Alisema Bwana WilliamVile vile alibainiaha kuwa, Huduma ya pili ni nyongeza ya asilimia 2 kwa wastaafu wote wanaolipwa zaidi ya Shilingi 150,000 kwa mwezi, Nyongeza hiyo itasaidia pensheni ya wastaafu kuendana na mabadiliko ya mfumuko wa bei.Fao la msaada wa mazishi la Shilingi 500,000litakalo lipwa kwa familia ya mstaafu aliyefariki. Fao hilo linalipwa haraka ili kusaidia familia kugharamia taratibu za mazishi kwa heshima, pamoja na malipo ya mkupuo wa miezi 36 kwa wategemezi wa mstaafu aliyefariki.Chini ya utaratibu huo, wategemezi watalipwa jumla ya pensheni ya miezi 36 aliyokuwa akiipata marehemu kwa awamu moja, badala ya kusitishwa mara baada ya kifo.Aidha amefafanua kuwa utaratibu wa malipo ya miezi 36 na fao la mazishi ulianzishwa Julai 2022 kwa wastaafu waliolipwa kwa mfumo mpya wa ukokotoaji bora wa mafao, na sasa umepanuliwa kuwajumuisha wastaafu wote wa mifuko iliyounganishwa kuunda PSSSF.Hata hivyo ameeleza kuwa huduma hizo nne zitaendana na maboresho ya kidijitali kupitia mifumo ya PSSSF Kiganjani na TeHEMA, ambapo wanachama na wastaafu wanaweza kufuatilia michango, kuwasilisha maombi na kupata huduma bila kufika ofisini..

PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment