Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi, ameendelea na kampeni ya Ongea na Kamanda ambapo leo ilikuwa zamu ya Kata ya Burige Halmashauri ya Msalala.Akiongea katika kampeni hiyo Kamanda Magomi aliwashukuru wananchi kwa kujenga kituo cha Polisi katika eneo hilo na kuwaambia wananchi hao kuwa kitakapokamilika kitasaidia kutatua changamoto ya kufuata huduma za Polisi umbali mrefu.Kamanda Magomi aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aliendelea kuhimiza wananchi kutovumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia badala yake wavitolee taarifa ili hatua stahiki zichukuliwe.Aliendelea kuwakumbusha usalimishaji wa silaha haramu zinazomilikiwa na wananchi na kuwa kampeni hiyo inaelekea ukingoni kwani itaisha oktoba 31 mwaka huu na kusema baada ya hapo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote ambao watakutwa na silaha haramu.Kwa upande wa wananchi wa Kata hiyo walilipongeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana nao katika ujenzi wa Kituo hicho na kuomba kuletewa askari mapema ili kituo hicho kianze kazi mapema. Aidha Kamanda Magomi pia alitembelea Kituo hicho kuona kazi za ujenzi zikiendelea na kutoa tena pongezi kwa hatua nzuri iliyofikiwa

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment