
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Chemba, imefanikiwa kushinda kesi ya uhujumu uchumi iliyomhusu Thabiti Yusufu Ngulungu, aliyekuwa Afisa Hesabu Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na ambaye kwa sasa ni Afisa Hesabu Msaidizi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa.
Mahakama ya Wilaya ya Chemba, Oktoba 20, 2026, imemtia hatiani Ngulungu kwa kosa la wizi wa fedha za mauzo ya viwanja kiasi cha Shilingi 3,600,200.
Ilielezwa mahakamani kuwa kati ya Januari 8 na Desemba 30, 2020, mshtakiwa alipokea fedha za mauzo ya viwanja kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mombose, John Wenga, lakini aliwasilisha kwa Mtunza Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba fedha pungufu ya kiasi kilichopaswa kuwasilishwa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment