
Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam
Teknolojia imeendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwemo matumizi ya mfumo wa kidijitali unaomwezesha mgonjwa kujisajili mwenyewe, kuchagua daktari anayemtaka na kupata huduma kwa wakati aliochagua.
Akizungumzia ubora wa huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo katika kuhitimisha wiki ya huduma kwa mteja Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI inaendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa wagonjwa huku ikiendelea kuwajali na kuwafuata pale walipo.
Dkt. Kisenge alisema Taasisi hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa kutoka nchi zaidi ya 20 hatua inayotokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika miundombinu na wataalamu.
Aidha Dkt. Kisenge alisema utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo umeonesha kuwa zaidi ya asilimia 97 ya wagonjwa wanaotibiwa hapo wameridhishwa na huduma zinazotolewa katika ngazi zote za kutoa huduma.
Kwa upande wao wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo walisema matumizi ya mfumo wa kidijitali katika Taasisi hiyo yamerahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati bila ya kulazimika kukaa foleni kwa muda mrefu.
Joyce Elias alisema kupitia huduma hiyo mgonjwa anaweza kufika hospitalini kwa wakati aliochagua na kumuona daktari moja kwa moja, hatua hiyo inalenga kuwajali wateja na kutoa huduma iliyo bora.
“Wataalamu wa JKCI wanafanya kazi kwa pamoja na kuwa na mawasiliano ya pamoja, hali inayomrahisishia mgonjwa kupata huduma kwa urahisi katika kila hatua anayopita”, alisema Joyce
Seif Abdallah alisema kupitia mfumo wa kidigitali huduma za ufuatiliaji wa wagonjwa zinaendelea hata wanapokuwa nyumbani ambapo madaktari huwapigia simu wagonjwa kufuatilia hali zao na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya dawa walizopewa.
Naye Margareth Christopher alisema huduma kwa wateja katika taasisi hiyo ni nzuri kwani wagonjwa wanapofika hupata huduma kwa wakati bila kusubiri kwa muda mrefu.
“Mbali na kuhudumiwa kwa wakati Taasisi hii imeongeza utaratibu wa kutupatia wagonjwa viburudisho kama vile kahawa tunaposubiri kupata huduma jambo linalotufanya tujisikie kama tupo nyumbani”, alisema Margareth.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment