NA: DK. REUBENI LUMBAGALA
Maendeleo katika sekta yeyote yanategemea kwa kiasi kikubwa utashi wa kisiasa walionao viongozi. Pale ambapo viongozi wametanguliza dhamira ya dhati katika kufanikisha jambo fulani, basi jambo hilo ni lazima litafanikiwa.
Sekta ya maji ni miongoni mwa sekta muhimu zenye mchango mkubwa wa kuharakisha maendeleo nchini. Sekta hii imefungamanishwa na sekta nyingine za kimaendeleo ambapo mafanikio yake ni nyenzo ya mafanikio ya sekta nyingine.
Mathalani, sekta ya kilimo inategemea upatikanaji wa maji ambayo husaidia kukuza mazao na hatimaye usalama wa chakula hupatikana na hali za maisha ya wakulima hubadilika na kuwa nzuri zaidi.
Halikadhalika, katika sekta nyingine kama uvuvi, mifugo, ujenzi, viwanda, elimu, afya, kutaja kwa uchache, hutegemea maji ili kuleta ubora na ufanisi wa uendeshaji wake.
Tangu akiwa Makamu wa Rais na sasa Rais kamili, Dk. Samia Suluhu Hassan ni mdau na mkereketwa mkubwa wa sekta ya maji. Ni kiongozi mwenye maono ya kutaka kila mwananchi awe anaishi mjini au kijijini, awe maskini au tajiri, apate huduma bora ya maji na ya uhakika ili kuendesha shughuli za kila siku.
Si hivyo tu, Rais Dk. Samia anataka kuona wananchi wanapata maji katika makazi yao na kuepuka kadhia ya kutembea umbali mrefu ili kuyapata maji. Ni kwamba, anataka muda wa kutafuta maji utumike katika shughuli za maendeleo kama kilimo na biashara ili nchi yetu isonge mbele zaidi kimaendeleo.
Aidha, anataka baadhi ya migogoro ya ndoa inayotokana na wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji iishe kwa maji kupatikana karibu na makazi ya wananchi na ndiyo maana anapigania kumtua ndoo mama kichwani.
Si hivyo tu, anataka wakulima walime kilimo cha uhakika ikiwezekana hata mara tatu kwa mwaka kupitia umwagiliaji kwa kuhakikisha mabwawa na visima vinakuwepo ili wananchi wajiongezee kipato kupitia kilimobiashara cha umwagiliaji.
Kiufupi, Rais Dk. Samia anataka maji yawe nyenzo ya uchumi hasa kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, badala ya kudhani maji ni kwa ajili ya kunywa, kuoga na kufua nguo tu.
Kutokana na hayo, Rais Dk. Samia amekuwa akiiwezesha Wizara ya Maji, fedha nyingi za kugharamia miradi ya maji ili kuongeza mtandao wa upatikanaji wa maji nchini, na hivyo kufanikisha azma ya serikali ya kuwapatia wananchi wake maji safi, salama na yenye kutosheleza. Kwa mfano, kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara ya Maji iliidhinishiwa shilingi trilioni 1.12.
Kutokana na utashi mkubwa wa kisiasa aliouonyesha Rais Dk. Samia katika sekta ya maji, Oktoba 22, 2026, Jijini Luanda, nchini Angola, katika mkutano wa viongozi wa Afrika, serikali ya Tanzania ilipongezwa kufuatia mafanikio ya uwekezaji katika sekta ya maji. Mkutano huo mkubwa umehusisha marais, mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa maji kujadili namna raslimali za maji zinavyoweza kujenga amani.
Ikumbukwe kuwa, kwa sasa, hali ya upatikanaji wa maji nchini imeimarika sana katika maeneo ya mijini na vijijini, huku mkakati uliopo ni kufikisha maji katika vijijini 1,575 vilivyobaki kati ya vijiji 12,333, ifikapo mwaka 2030.
Kwa hakika, utashi wa kisiasa na juhudi za Rais Dk. Samia katika sekta ya maji kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo, zimeonyesha matokeo chanya na kutambuliwa rasmi katika mkutano nchini Angola na kuwa somo zuri kwa nchi nyingine barani Afrika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment