Wawekezaji wametakiwa kutumia bima ili kuwa na uhakika wa mali zao katika vipindi ambavyo hutokea misukosuko inayotokana na majanga yanajitokeza na kuleta hasara.
Msuluhishi Mkuu ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) Aloyce Mbunito alisema jana kwenye hitimisho la Maonesho ya Tisa Kitaifa ya Teknolojia ya Madini katika mji wa Geita alisema kuna usalama wa kutumia bima katika ulinzi wa mali.
Alisema idara yao hutatua migogoro ya bima kwa kutumia njia mbadala nje ya utaratibu wa kawaida wa kimahakama kwa haraka na bei nafuu.
Mbunito aliongeza kusema kuwa humlinda mtumiaji wa huduma za.bima na soko la bima hivyo kujenga na kukuzanumani ya umma kwenye biashara ya bima.
Mtathimini Bima Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa Jerry Mwantuke alisema upo usimamizi mzuri unofanywa na idara hiyo kuhakikisha idara hiyo inafanya vizuri ili watanzania watumie kukinga mali zao.
Alisema bima wanazosimamia zinaenenda kwa utaratibu wake ili kuwezesha ufanisi katika kutoa huduma kwa watanzania.
Naye Ofisa Uhusiano Bodi ya Bima ya Amana; Pius Makulilo alisema bodi huwalinda wenye amana wadogo kutokana na athari za kupoteza amana zao pale benki au taasisi ya fedha inapofilisika ili kujenga imani ya watanzania katika mfumo wa fedha nchini.
Alisema kuna amana ya kinga kwa fedha zinazowekwa na wafanyabiashara katika mabenki hapa nchini ambayo kwenye Bodi ya Bima ya Amana.
Post a Comment